Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (AS) –ABNA-, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, amepongeza ujumbe wa hekima na msukumo uliotolewa na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, akisema utakuwa mwongozo mkuu katika hatua za Iran za baadaye.
Katika taarifa yake aliyomuelekeza Kiongozi wa Mapinduzi, Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei, Qalibaf alisema kuwa maelekezo hayo yameweka wazi kuwa kutiwa saini kwa waraka wa makubaliano si mwisho wa safari, bali ni mwanzo wa hatua ngumu za kurejesha haki za wananchi wa Iran na Kambi ya Muqawama kutoka kwa adui anayekiuka ahadi zake.
Aidha, alisisitiza kuwa Bunge la Iran litayafanya maelekezo ya Kiongozi wa Mapinduzi kuwa dira yake, na halitaruhusu upande mwingine kutumia ukiukaji wa makubaliano au vitisho kuhujumu haki za taifa la Iran na Kambi ya Muqawama. Pia alieleza kuwa ujumbe huo umeimarisha uwezo wa Iran wa kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa ahadi na wajibu wa Marekani chini ya makubaliano hayo.
Your Comment